Loading

kurudi nyumbani FARU MWEUSI WA MASHARIKI <|> DICEROS BICORNIS MICHAELI

Grumeti Fund inaadhimia kuchangia kuongeza idadi na kulinda spishi ya Faru weusi wa Afrika Mashariki walio hatarini kutoweka ndani ya Ikolojia ya Serengeti. Kwa kushirikiana na wadau wetu wa serikali ya Tanzania, tunafanikisha kuhamisha na kuwarejesha upya faru weusi kwenye makazi yao ya awali kaskazini mwa Tanzania.

Ulinzi ni muhimu kwenye kumlinda faru mweusi aliyopo na atakaetambulishwa. Mifumo iliyopo na teknolojia vitaimarishwa kutekeleza hatua mahsusi za usalama wa faru.

Kundi la Oparesheni maalumu, pamoja na kitengo cha mbwa, huunda sehemu muhimu ya mpango wa usalama.

Mfumo wa ufahamu wa kikoa hukusanya taarifa zote. Uwezo wa kukusanya na kuoanisha taarifa kwa muda ni muhimu.