Sisi UVIMA SACCOS ni nani?
UVIMA ni kifupi Cha maneno Umoja wa Vikundi Marangu
Hii ni Taasisi ya Kifedha (SACCOS) iliyoanzishwa mwaka 2007
Chama hiki Cha Usharika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kilianzishwa baada ya wanachama waliokua ndani ya vikundi vya VICOBA kuungana kwa hiari yao wenyewe
Kwa sasa SACCOS hii inahudumia mtu yeyote au Vikundi ili Mradi wakidhi hitaji la fungamano letu
Mwaka wa Fedha wa UVIMA SACCOS LTD
Upangaji wa kimkakati wa kifedha huhakikisha uthabiti, ukuaji na usalama wa muda mrefu.
Ofisi na Makao Makuu ya UVIMA SACCOS
Fungamano letu (Common Bond)
Ni Mfungamano wa pamoja wa Wanachama wa UVIMA wanaopatikana ndani ya Wilaya ya Moshi ikiwemo vikundi na watu binafsi ambao wengi wao ni wafanyakazi, wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wadogo wadogo.
Madhumuni ya Chama
Kuondoa umaskini na kukuza kipato cha Wanachama kwa kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika.
Dhima (Mission)
Kuwa Chama imara cha Ushirika chenye kutoa huduma bora za kifedha ili kuboresha maisha ya jamii Masikini iishiyo vijijini.
Dira/ Njozi Yetu (Our Vision)
Kuwa taasisi bora ya kifedha inayoboresha maisha ya jamii masikini iishiyo vijijini kwa kufanya yafuatayo;
Kutoa elimu ya ushirika kwa wananchi ili waweze kujiunga kwenye SACCOS yetu ya UVIMA
Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi na wanachama ili waweze kutumia fursa zilizopo na kujikomboa na umaskini
Lengo Kuu (Main Objective)
Lengo kuu ambalo chama kinatarajia kufikia ifikapo mwishoni mwa 2025 ni kuwa na mtaji unaotosheleza mahitaji ya mikopo ya wanachama
Malengo mengine ni pamoja na;
Kuwezesha wanachama wake kuweka akiba na kukopa mikopo kwa masharti nafuu kabisa
Kuviunganisha vikundi vya VICOBA, vikundi vya wajasiriamali na wanachama wake na kuvisimamia
UONGOZI NA MENEJIMENTI YA UVIMA SACCOS LTD
Tafadhali tembelea kurasa zetu👇
Credits:
SACCOS Bora Mkoani Kilimanjaro